Lesson 1 of 4 · Grade 7 Kiswahili
Aina za maneno
15 min
Kuna aina nane za maneno katika Kiswahili:
- Nomino (N): majina ya watu, vitu, mahali. Juma, kitabu, Mombasa.
- Kiwakilishi (W): husimama badala ya nomino. yeye, sisi, hiki.
- Kitenzi (T): huonyesha tendo. soma, cheza, lala.
- Kivumishi (V): hueleza nomino. -zuri, -refu, hiki.
- Kielezi (E): hueleza kitenzi. haraka, polepole, jana.
- Kihusishi (H): huonyesha uhusiano. juu ya, chini ya, kwa.
- Kiunganishi (U): huunganisha. na, lakini, ili.
- Kihisishi (I): huonyesha hisia. Lo! Ala! Ah!
Mfano: Lo! Mtoto mdogo alikimbia haraka.
- Lo! (I), Mtoto (N), mdogo (V), alikimbia (T), haraka (E).
Key points to remember
- Aina nane za maneno
- Kielezi hueleza kitenzi
- Kihisishi huonyesha hisia
- Kihusishi huonyesha uhusiano
Test yourself